Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na Taasisi ya Viwango Tanzania TBS kwa pamoja wanakaribisha wazalishaji wa bidhaa nchini kushiriki katika uzinduzi wa kampeni ya Fahari ya Tanzania'-Proudly Tanzania Campaign' ambayo itakwenda sambamba na utoaji tuzo wa Bidhaa 50 bora za Kitanzania-Top 50 Tanzania Brands Awards 2016.

Kampeni hizi na utoaji tuzo utahudhuriwa na Mh. Samia suluhu Hassani, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Viwanda, Biaashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage Viongozi mbalimbali pamoja wageni waalikwa wapatao 400 sherehe zitakazofanyika Tarehe 20 Septemba 2016 katika ukumbi wa Mlimani City.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya uzinduzi wa kampeni hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Sembeye amesema Fahari ya Tanzania ina malengo makuu manne ambayo ni kuhamasisha uzalishaji unaotumia viwango vya ubora ili kukidhi matakwa ya soko.

Amesema kuhamasisha utumiaji wa bidhaa za nchini zilizokidhi ubora na viwango stahiki, kuhamasisha wazalishaji kuongeza dhamani ya bidhaa au kuzalisha kwa kutumia malighafi za Kitanzania. Pia amesema kuhamasisha ushindani wa kuuza kwenye masoko ya nje.

Simbeye amesema kuwa katika kuzindua kampeni hii TPSF, TBS na washirika wao waliona kuanza kwanza na utambuzi wa Bidhaa 50 bora za Kitanzania.

Kwa upande wa Msimamizi wa Kampeni hizo, Emmanuel Nnko amesema kwenye tuzo hizo zitakuwa na madaraja mawili ambayo ni Premier linalohusu Wafanyabiashara au Makampuni makubwa na daraja la wajasiriamali wadogo kama special category. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini, Gofrey Simbeye akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea uzinduzi wa Kampeni endelevu ya Fahari ya Tanzania pamoja na utoaji tuzo kwa Bidhaa 50 za Kitanzania, sherehe zitakazofanyika tarehe 20 Septemba 2016 katika ukumbi wa Mlimani City Conference. Kulia ni Msimamizi wa Kampeni hizo, Emmanuel Nnko.  Msimamizi wa Kampeni za endelevu ya Fahari ya Tanzania pamoja na Utoaji Tuzo kwa Bidhaa 50 za kitanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...