Mwenyekiti  wa Chama cha CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe


Na Anthony John,
Globu ya Jamii
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kimesitisha  shughuli  zote  za maandamano na mikutano nchi nzima,kwa kudai kuwa ukuta ni fikra endelevu na si mpango wa siku moja.
 Hayo yamesemwa leo na  Mwenyekiti  wa Chama hicho Taifa,Mh.Freeman Mbowe wakati  akizungumza  na Waandishi  wa Habari,Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Mbowe amesema kuwa wataendelea Kujipanga katika kulinda  Haki yao ya kidemokrasia kama ambavyo katiba ya vyama vya siasa inavyosema,kuwa ni haki yao ya kidemokrasia.
‘’Mapambano  ya  kisiasa si tukio la siku moja ni tukio endelevu na kwa hiyo tarehi Mossi ,Oktoba ambayo ilikuwa ni siku mbadala ya maandamano maalum,hivyo kwa niaba ya kamati kuu imeona kuna umuhimu  wa kusimamisha maandamano maalumu na mikutano nchi nzima ilikupisha mbinu nyingine mbalimbali’’amesema Mbowe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Njaa zinasumbua sana vichwa vya watu. Angalau leo umempa sekunde 20.

    ReplyDelete
  2. Hizo njaa zisituchafulie nchi basi. hawa jamaa wa kusini wana agenda nyingine. Mbona Moshi mjini kutulivu na hawafanyi fujo huko?

    ReplyDelete
  3. hakuna maandamano. Mnatishia nyau tingatinga?? Acheni kuwaongepea wananchi hakuna cha maandamano.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona magazeti ya Tanzania yanapenda uchochezi baina ya serikali Na upinzani baada ya kuandika maneno ya kuwapongeza wanatia vitina sio sawa

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...