Na: Frank Shija, MAELEZO 


 Ukubwa wa deni la taifa siyo jambo linaloweza kusababisha kuyumba kwa uchumi wa nchi, kinachooneka ni kuendela kuaminiwa kwa Tanzania ndani na nje ya nchi jambo linalopelekea tuna pata fursa ya kukopesheka kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 

Hayo yamebainishwa na Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi, Profesa Haji Semboja alipofanya mahojiano maalum na mwandishi kutoka Idara ya Habari, MAELEZO kuhusu hali ya uchumi ilivyo kutokana na ongezeko la deni la Taifa leo Jijini Dar es Salaam. 

“Ukubwa wa deni la taifa siyo mzigo mbaya, ni mzigo wa kimaendeleo. Unnecessary devil” Alisema Profesa Semboja. 

Aliongeza kuwa kutokana kwa imani waliyo nayo wahisani ndani na nje ya nchi ndiyo maana washirika wetu wanatukopesha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama ambavyo tumeshuhudia ujenzi wa Daraja la Kigamboni, hivi karibuni tutanufaika na usafiri wa ndege”. Alisema Profesa Semboja. 

Aidha amempongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. Jonh Pombe Joseph Magufuli kwa hatua alizochukua za kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuondoa safari za nje zisizo za rasmi pamoja na kupiga vita vitendo vya rushwa. 

Semboja aliendelea kusema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni Serikali ya awamu ya Tano kulipa madeni ya watangulizi wake huku ikitekeleza miradi ya maendeleo jambo linaloongeza imani miongoni mwa wahisani. 

Hata hivyo alionya juu ya matumizi mabaya ya rasilimali fedha kuwa zinasababisha kushindwa kutekeleza wajibu wa kulipa deni kwa wakati na kupelekea kulimbikiza madeni jambo ambalo si sahihi. 

Alitajaa baadhi ya matumizi mabaya ya fedha kuwa ni pamoja na safari za nje na ndani ya nchi zisizokuwa na tija, ulevi, kupelekea fedha katika miradi isiyopangwa na mengine. 

Wananchi wametakiwa kutoyumbishwa na waelewi kuwa kupitia fedha zinazokopwa wanufaika wakuu ni wananchi wenyewe, mfano fedha zitakazo tumika kujenga Nyumba za Magomeni ambazo Mhe. Rais amehaidi waliokuwa wakazi wake kuishi bila kulipia kwa kipindi cha miaka mitano zikitokana na mikopo hiyo wananufaika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Prof mkweli lakini kwa asilimia 50 tu. yapo mazingira ambapo deni la taifa lina madhara kwa jamii. yeye kama msomi alitakiwa aeleze ni katika mazingira yapi deni kubwa halina madhara kwa taifa na wakati gani deni lina madhara. mwalimu nyerere alizunguka dunia nzima akibembeleza nchi masikini zifutiwe madeni, sasa leo huyo Prof anatuambia ati kuwa na deni kubwa ni dalili nzuri?!!!

    ReplyDelete
  2. Michuzi, Ni muhimu kueleza ni Semboja yupi aliyetoa taarifa hii maana picha iliyowekwa ni tofauti na jina la aliyetoa maelezo.

    ReplyDelete
  3. waoga wa kuongea ukweli.
    anatakiwa aeleze faida na madhara yake..

    ReplyDelete
  4. Dear Michuzi,
    Picha ya mtu uliye muweka kwenye hii makala yako sio huyo uliye mtaja kwenye makala hiyo. Prof. Haji Semboja ni mtu tofauti na Prof Jesephat Semboja. Aliye kwenye picha ni Prof. Josephat Semboja na sio Haji Semboja.
    Thafadhali ongeza umakini.

    ReplyDelete
  5. Siyo kweli, hiyo picha ni ya Prof. Haji Sembaja kwa uhakika kabisa. Ni mwalimu wangu Chuo Kikuu cha Dae es Salaam

    ReplyDelete
  6. Sasa picha inaendana na mtoa maelezo. Asante kurekebisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...