Na Anthony
John, Globu ya jamii.
Mwenyekiti wa
Jukwaa la Wanahabari,Theophil Makunga ameipongeza Serikali kwa niaba ya
wanahabari kwa kuanza mchakato kuondoa Sheria ya Magazeti ya mwaka1976 kwani
Sheria hiyo amedai ilikuwa inawabana wanahabari. Pia akifafanua kuwa,serikali
imeanza mchakato wa kubadilisha Sheria hiyo ya Magazeti iliyo kuwepo kwa
Miaka 40 tangu ianze kutumika,hivyo alisema Sheria itakayo anzishwa itafanya
kazi kwa muda mrefu kwa Miaka 40 hadi 50.
Serikali
imesikiliza kilio cha wanahabari na imeanza mchakato wa kubadilisha hiyo
Sheria,sasa kwa sababu hiyo kama alivyosema katibu ni kwamba Sheria hiyo imekaa
kwa muda wa Miaka 40 kwa hivyo hata mpya itakayotugwa sasa itakaa Miaka 40 hadi
50 inayokuja.
Hivyo
Hivyo,Katibu Mkuu wa Jukwaa la wanahabari Neville Meena amesema watapata maoni
ya wadau mbali mbali wa Habari kupitia klabu za waandishi wa habari watakao
kwenda kuwaeleza maudhui yaliyomo ndani ya Sheria yenyewe ilikupata maoni yao
wenyewe vila kuwashawishi.
"Maana
yake tukienda kufanya uchambuzi watachukua maoni yetu kama maoni yao, hata
hivyo tumekuwa tukipokea lawama nyingi kutoka kwa waandishi kutokushiriki na
wakati wao ndio wako kwenye vyombo vya Habari" hayo,"amesema
Meena.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanahabari Bw. Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuipongeza Serikali kwa niaba ya wanahabari kwa kuanza mchakato wa kuondoa Sheria ya Magazeti ya mwaka1976 kwani Sheria hiyo ilikuwa inawabana wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wanahabari, Bw. Neville Meena.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...