Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida, akionyesha sehemu ya msaada uliotolewa na Serikali ya Japan leo jijini Dar es Salaam, ukishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira akizungumza na waandishi wa habari wa kupokea msaada wa dola za kimarekani milioni 1.8 kwa ajili ya kununulia chakula cha wakimbizi zaidi ya 200,000 ambapo msaada huo unakwenda shirika la lisilo la serikali leo jijini Dar es Salaam.
Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii.
WAKIMBIZI zaidi 200,000 walio katika Mikoa ya Kasikazini na Magharibi nchini wapwa msaada wa chakula kilichogharimu Dola za Marekani Milioni 1.8 kutoka serikali ya Japan.
Msaada huo umeshudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira wakati wa mkabidhiano ya msaada kutoka kwa Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida, pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Tanzania.
Balozi wa Japan amesema kuwa msaada huo kwa serikali ya Tanzania ni wa kiubinadamu wa kukubali kuwa na wakimbizi.
"Serikali ya Japan imefurahishwa na utoaji wa fedha hizo kwa ajili ya msaada wa chakula kwa wakimbizi walioko nchini Tanzania kutokana na wakimbizi kukosa chakula na hali ya duni ya lishe."
Kwa juhudi ambazo zinafanywa ni kutaka kuboresha upatikanaji wa chakula kwa maisha ya wakimbizi waendelee kukaa kwa amani katika mikoa ya kaskazini na magharibi mwa Tanzania.
Amesema fedha hizo ni sawa na bidhaa tani 1,800 ambazo zimetolewa na serikali ya Japan ikiwa ni virutubishi vya mafuta, pamoja na tani za mahindi 1,100 pia manunuzi ya vyakula vya virutubishi vya uji kwa ajili ya wakina mama na watoto walio katika hatari ya kupata utapiamlo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...