Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella (kulia) akishuhudia mojawapo ya mechi za Vodacom Premier League katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara , “Vodacom Premier League” imesikia kilio cha mashabiki na wapenzi wa soka nchini na kuamua kuwaletea kifurushi maalumu kinachojulikana kama ‘Soka bando’ ambacho ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote.
Vodacom Tanzania imebuni kifurushi hiki kwa ajili ya kuwapatia taarifa za soka za hapa nchini na ligi za kimataifa kwa gharama nafuu ya shilingi 500/-Kifurushi cha ‘Soka bando’ kitakuwa kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa saa 24. 
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyombella amesema “Kwa gharama nafuu ya shilingi 500/-mashabiki wa soka wanaotumia mtandao wa Vodacom watapata taarifa  mbalimbali za soka za hapa nyumbani na kimataifa kwa kipindi cha siku 7,dakika 14 za muda wa maongezi Vodacom kwenda Vodacom, dakika 2 za muda wa maongezi kwa mitandao  yote na jumbe fupi za maneno (SMS) 20 kwa kipindi cha masaa 24”
Alisema Vodacom Tanzania imeleta kifurushi hiki cha ‘Soka bando’ kipindi hiki ambacho msimu wa ligi ya VPL unaendelea ni furaha kwa Mtandao wa Vodacom kuwawezesha mashabiki kupata taarifa za ligi kwa urahisi kupitia mtandao wake ikiwemo kuwapatia burudani wateja wake na watanzania wote kwa ujumla.
“Kampuni inathamini na kutambua mchango wa mashabiki katika kukuza ligi hii tangu ilipoanza kuidhamini hivyo ndio maana tumewaletea kifurushi hiki ili wapate  burudani na taarifa za soka kwa wakati na kwa gharama nafuu”.Alisema Mwiyombella.
Ili kununua kifurushi hiki anachotakiwa kufanya mteja ni kupiga  namba *149 * 01#, na kuchagua ‘Soka Bando’. Baada ya  hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga”  “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460.Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya  Mspoti.vodacom.co.tz.
Wateja watakaojiunga na huduma hii pia watapata  nafasi ya kufurahia ofa na zawadi mbalimbali kutoka  Vodacom kama vile muda wa bure wa maongezi, sms au  MB za akuperuzi inteneti hususani timu wanazoshabikia zitakapokuwa zimeibuka na ushindi wa mchezo.
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania  bara unaendelea  katika viwanja mbalimbali nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...