Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ( Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora ametoa wito kwa vyuo vyote nchini kuanzisha mitaala inayohusu usalama wa mitandao ya mawasiliano ili kukabiliana na matumizi mabaya ya mitandao hiyo.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu huyo alipokuwa akifunga warsha ya siku ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola iliyohusu Uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama wa Mitandao iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Prof. Kamuzora amesema kuwa moja ya vitu vilivyoelezewa katika Sera ya Tehama iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu ni kuhakikisha mitandao ya mawasiliano inakuwa salama hivyo kila mwananchi anawajibu wa kulinda mitandao hiyo.

“Suala la usalama wa mitandao ya mawasiliano linapelekea kuwepo kwa fursa nyingi za ajira hivyo, napenda kutoa wito kwa vyuo mbalimbali nchini kuanzisha mitaala mipya itakayohusu masuala haya kwa sababu watu watatakiwa wajikite kwenye masomo yanayohusiana na mitandao”, alisema Prof.Kamuzora.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni zimebainisha kuwa dunia nzima inapoteza jumla ya dola bilioni 400 kwa mwaka kwa njia ya wizi wa mitandaoni hivyo kushindwa kulinda mitandao ya mawasiliano kunapelekea hasara kubwa kwa Taifa na Dunia kwa ujumla.

Naye Afisa Mwandamizi wa ufundi na ushauri wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola , Fargani Tambeayuk amesema kuwa Jumuiya hiyo inawasaidia nchi wanachama katika kudhibiti usalama wa mitandao ili kusaidia nchi hizo kupata maendeleo kwa kutumia mitandao pamoja ma kuepukana na uhalifu.

Kwa upande wake Mratibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Makosa ya mitandao, Joshua Mwangasa amesisitiza suala la kutolewa kwa elimu ya usalama wa mitandao liwe endelevu akiamini kuwa elimu hiyo itawasaidia wananchi kuepuka kutumia vibaya mitandao ya mawasiliano.

Aidha, ameusifia mpango huo kwani utawasaidia Jeshi la Polisi kuweza kukabiliana kirahisi na wananchi wanaofanya makosa kwenye mitandao pia amesisitiza kuwa makosa ya kimtandao ni kama makosa mengine hivyo taratibu za kuripoti makosa hayo ni zile zile za kawaida.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora akizungumza wakati akifunga warsha ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola (hawapo pichani) kuhusu uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao nchini. 
Afisa Mwandamizi wa ufundi na ushauri wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Bw. Fargani Tambeayuk akitoa shukurani kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na wadau wengine baada ya kumalizika kwa warsha ya uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Shabani Pazi akizungumza wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati wa kufunga Semina ya Uuandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama katika Mitandao leo. Jijini Dar es Salaam. 
Wadau wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati wa kufunga warsha ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola wanaoandaa mkakati huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...