Kundi la wasanii
wanane wa Kitanzania waishio nchini Unigereza (Wasanii Tanzania Uingereza - WASATU) waliwakilisha wenzao Jumatano iliyopita katika kikao na
Balozi mpya wa Tanzania nchini humo Dkt. Asha-Rose Migiro.
Kikao hicho kilichoitishwa na mheshimiwa Balozi
kilikuwa na madhumuni ya kuweka
ushirikiano kati ya jumuiya ya wasanii na Watanzania na Ubalozi huo. Balozi Migiro alisisitiza kuwa sera ya awamu
ya tano ni kuipa sanaa kipaumbele ili kuchangia maendeleo yetu ndani na nje.
Wasanii hao
walioongozwa na mcheza sarakasi na mwanamuziki Fab Moses walijitolea bila
malipo yeyote – wengine kutoka safari za mbali sana.
WASATU ilisisitiza haja ya kujituma zaidi kujenga sanaa na
mawasiliano na kusaidiana kujuana kuendeleza fani hii muhimu.
Kutoka kushoto ,
Rama Sax – aliyekuwa bendi ya Simba wa Nyika zamani, Saidi Kanda aliyepiga na
marehemu Remmy Ongala, Hamida Mbaga wa All Things African, Khadija Ismail wa
Kibisa na Muungano ya enzi hizo, Balozi
Dkt Asha Rose Migiro, Neema Kitilya anayetangaza mapishi ya Kitanzania Uingereza
na mwanamuziki Msafiri aliyewahi kuwa na African Stars band wana Twanga Pepeta ambaye siku hizi anatumia jina la Diouf Lewandowski. Waliochuchumaa mbele ni Freddy
Macha na Fab Moses
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na msanii Hamida Mbaga wa All Things African
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na msanii, mwandishi na mwanaharakati wa utamaduni Freddy Macha
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na
mwanamuziki Msafiri a.k.a Diouf Lewandowski
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro akiongea na wasanii hao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...