Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiandika baadhi ya hoja kutoka kwa baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa  kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.
baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi.

Na Fredy Mgunda, Ileje

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje, Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.

Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.

Mnasi aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.

Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

“Nawatahadharisha kwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mitihani hiyo, kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani na sipo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu yenu”alisisitiza Mnasi.

“hakikisheni kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo nawataka wasimamizi wote kufanya kazi kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu, pia nawaasa ndugu zangu kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,” alisema Mnasi.

Mnasi alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.

Aliongeza kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichopo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.

Nao wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa mitihani walizopewa.

mitihani hiyo ya kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...