Watanzania waishio
eneo la Bay area- Northen California, jana kwa pamoja walikusanyika katika kanisa la
Lutheran Oakland ili kukusanya michango ya
waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea kanda ya ziwa nchini Tanzania, hususan
mkoani Kagera ambako madhara makubwa yamerekodiwa.
Jumla ya dola za Kimarekani
4,000 za ahadi na fedha taslim zilipatikana hiyo jana.
“Tuna mpango wa kukusanya pesa zote ifikapo Jumamosi Septemba 24, 2016 na kuzituma Jumatatu Septemba 26, 2016 katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kagera ambapo shughuli zote uratibu na
makusanyo yote yanaelekezwa pale kama serikali ilivyoagiza” amesema Bw.
Erick Byorwango, Katibu mwenezi wa Jumuiya ya
Watanzania - Northern California.
Bw. Byorwango ameongeza kusema kuwa jitihada za kukusanya michango zinaendelea na
mwitikio wa mkutano huu ulikuwa na matumaini.
"Tunaomba mungu aendelee kutupa
nguvu na upendo ili tukamilishe zoezi hili na hatimaye tuwakilishe msaada wetu
serikalini" amemalizia.
Mchungaji Chussi akiongoza sala kabla ya kuanza mkutano wa Watanzania waishio eneo la Bay area- Northen California nchini Marekani waliokutanika jana kukusanya michango ya waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea kanda ya ziwa nchini Tanzania
Wajumbe wakiendelea na kikao
Sehemu ya watoto wa Watanzania waishio eneo la Bay area- Northen California
Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania waishio eneo la Bay area- Northen California Dr Mathias Kaaya akiongoza kikao.
Mimi nipo in the Bay Area na ni Mtanzania pia. I wish I could get in touch with the rest of the Tanzanians and see how I can donate as well.
ReplyDelete