Na Mathias Canal, Singida
Jumla ya wakazi 283 wa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida wakiwemo
wanaume 71 na wanawake 83 sawa na asilimia 29% wamejitokeza kupima
Virusi vya Ukimwi VVU ambapo wananchi wanne sawa na asilimia 1.4% kati
yao ndio waliokutwa na maambukizi hayo ambapo wanaume ni wawili na
wanawake ni wawili.
Mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye mapambano
dhidi ya UKIMWI zina ujumbe usemao Tanzania Bila Maamubukizi Mapya chini
ya kauli mbiu ya "Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi inawezekana"
imekuwa ikiwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao
ili kurahisishia serikali kujua hali ilivyo ya maambukizi kama inapungua
ama inaongezeka ili kufahamu namna bora ya kuisaidia jamii kupunguza
maambukizi hayo yasiyo kuwa na lazima.
Akitoa taarifa hiyo wakati
akiwashukuru wananchi kwa kushiriki kwenye mkesha na shughuli nzima za
Mwenge wa Uhuru tangu ulipowasili Wilayani hapo jana asubuhi Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa Watanzania
wanaweza kuepuka vifo visivyo kuwa vya lazima pamoja kwa kupima na
kuzifahamu afya zao kwa itakuwa rahisi kwa wao kupatiwa dawa za kufubaza
makali ya Virusi vya Ukimwi jambo ambalo litawafanya kuishi muda mrefu
kuliko kuishi na Virusi vya Ukimwi kwa kificho kwani ni hatari kwa
mustakabali wa Maisha yao na kusababisha vifo vya haraka mara baada ya
kuathirika.
Hata hivyo Dc Mtaturu ameutaja ugonjwa wa Maralia
kuwa ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua watu wengi katika Wilaya
hiyo ambapo mwaka 2015/2016 ugonjwa huo uliongoza katika magonjwa kumi
ndani ya Wilaya.
Alisema kuwa wastani wa vifo katika Wilaya ya
Ikungi vilivyotokana na Maralia kwa Mwaka 2015/2016 ni watu 6 kwa upande
wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, wenye umri zaidi ya miaka
mitano ni wawili huku kwa upande wa wanawake kukiwa hakuna kifo
kilichoripotiwa.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa jumla ya
wagonjwa 35,408 waliugua Malaria, kati yao watoto wenye umri chini ya
miaka mitano ni 15,788 na wenye umri zaidi ya miaka mitano ni 19,620.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu George Jackson
Mbijima amewashukuru wananchi kwa umoja wao kwa kujitokeza kwa wingi
kwenye shughuli za Kukimbiza Mwenge huo kwani wameonyesha imani kubwa
tena kwa vitendo na serikali ya awamu ya Tano yenye kauli mbiu ya Hapa
Kazi Tu.
Mbijima alisema kuwa ni jambo la nadra sana kwa baadhi
ya wananchi kujitokeza kupima kutokana na Jografia pamoja na dhana ya
kuamini kuwa kujitokeza kupima ni kujiaibisha ama kurahisisha vifo
kutokana na mawazo mara baada ya kifahamu afya zao.
Sambamba na
hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Hassan Tati akitoa
salamu za Shukrani kwa niaba ya CCM amewapongeza wananchi kujitokeza
kwa wingi kuunga mkono Mwenge wa uhuru kwani ni dhahiri kuwa wameonyesha
kukiamini Chama Cha Mapinduzi CCM na serikali ya awamu ya tano kwa
kuenzi Nembo ya Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikimbia na baadhi ya watumishi wa Wilaya yake ishara ya kuukabidhi Mwenge wa uhuru Manispaa ya singida mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Ikungi
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Hassan Tati akizungumza wakati wa kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kupima Virusi Vya Ukimwi
Wananchi wa Manispaa ya Singida wakiusubiri Mwenge wa Uhuru kwa shauku kubwa muda mchache kabla ya kuwasili katika eneo lao ukitokea Wilaya ya Ikungi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...