Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipokea kiasi cha Shilingi Milioni 1.6 kutoka kwa Mratibu Taifa wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Bi. Mariam Kilembe wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kwa ajili ya Kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, leo Bungeni Mjini Dodoma.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 121.679 ili kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Jumamosi, Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.Msaada huo umetolewa leo (Ijumaa, Septemba 16, 2016) na wadau mbalimbali wakiwemo Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Caspian, Bw. Omid Karambech aliyetoa sh. milioni 100.

Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bordar Limited, Bw. Wu Yahui aliyetoa sh. milioni 20 pamoja na Bi. Mariam Kitembe aliyetoa sh. milioni 1.679 kwa niaba ya Wauguzi walioshiriki mafunzo ya Utafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).Akipokea msaada huo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Waziri Mkuu amewashukuru kwa michango yao ya fedha na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.

Jumapili, Septemba 11, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kagera ili kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo pamoja na kujionea madhara yaliyojitokeza.

Pia aliongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba kuaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko hilo. Aliwaomba wananchi wawe watulivu na kuwaahidi kuwa Serikali itakuwa pamoja nao.

Jumanne, Septemba 13 mwaka huu Waziri Mkuu aliongoza hharambee ya kuchangia waathirika wa teteme hilo na kupokea zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kitanzania.

Mbali na kusababisha vifo, watu wengine 253 walijeruhiwa na maelfu ya wananchi walikosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
  1. L. P. 980,
DODOMA.

IJUMAA, SEPTEMBA 16, 2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...