Na Ally Daud – Maelezo.
HOSPITALI  za Muhimbili, Amana, Mwananyamala na  Kairuki za Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuwekwa kwenye mradi maalum wa kudhibiti taka hatarishi ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha usafi wa mazingira katika huduma za afya nchini.

Mradi huo wa kudhibiti taka hatarishi ikiwemo sindano, gloves, nyembe na bandeji unasimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mazingira uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma ya Afya na Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Neema Rusibawengile  alisema kuwa lengo la mradi huo  una lengo la kukabiliana na magonjwa ya maambukizi katika maeneo ya hospitali nchini. 

“Mkutano huu umelenga kuandaa na  mradi utaodhibiti taka hatarishi amabao utanza kufanya kazi katika hospitali za Muhimbili,Amana,Mwananyamala kairuki na baadaye kuendelea nchi nzima” alisema Dkt Rusibawengile. 

Dkt. Rusibawengile alisema kuwa  mkutano huo pia umewakutanisha wadau mbalimbali wa Maendeleo na Mazingira watakaojadili   mbinu mpya za kutunza mazingira kwa ajili ya kupeuka magonjwa ya maambukizi nchini yanayotokana na taka hatarishi.

Kwa mujibu wa Dkt Rusibawengile alisema  mkutano pia huo unalenga kupata njia mbadala za kupunguza uzalishaji wa mekyuri katika hospitali, zahanati na vituo vya afya ili kuondoa utumiaji wa vifaa vyenye nishati hiyo.

Kwa upande wa mratibu wa udhibiti wa taka hatarishi za Hospitali Dkt. Honest Anicetus alisema  wadau wa mkutano huo pia wamepanga kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili  sekta ya afya katika utunzaji wa mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...