Mnyama Faru anakiakisi Jina la Kiingereza Rhinoceros ama FARU na sio KIFARU kama wengine waitavyo. Asili ya Jina hili la kiingereza limetoholewa kwenye lugha ya Kiyunani/Greece lina mashina mawili Rhino (Pua) na Ceros (Pembe) 

Faru ni miongoni mwa wanyama ambao ni BIG FIVE kwa Africa, wengine ni chui, simba, mbogo na tembo. Kuna takribani aina tano za faru duniani na Africa tuna aina mbili za faru ambazo ni WHITE RHINO na BLACK RHINO na aina nyingine tatu zilizobaki zinapatikana barani Asia, na kwa Tanzania sisi tuna aina moja tu ya Faru ambayo ni Black Rhino ingawa pia kuna White Rhino wanaopatikana Mkomazi ambayo ni introduced species waliochukuliwa kutoka South Africa. 
Faru 'mweupe' ni mamalia wa pili kwa ukubwa baada ya Tembo, huku kukiwa na spishi mbili za faru wapatikanao barani Afrika ambazo ni faru mweupe na faru mweusi. Utofauti wa faru hawa ni kwenye namna ya midomo yao ilivyo kaa na sio rangi kama wengi wananyodhani. Faru wa Afrika na Sumatra (ambao ndio wadogo lakini wakali sana) wana pembe mbili huku wale wa Uhindi na Java wakiwa na pembe moja tu. 

 Kwa kawaida faru ni wanyama ambayo huishi maisha ya mmoja mmoja (Solitary ) na dume na jike hukutana tu katika msimu wao wa ujamianaji ambapo kipindi hicho hutafutana kwa njia ya harufu ambayo hutolewa na jike pale anapokuwa anamuhitaji dume. 
Kwa bahati mbaya hivi sasa wanyama hao wamekuwa wakipungua kutokana na ongezeko la ujangili uliokithiri barani Afrika. Pembe ya Faru inasadikika kutumika kama tiba ya magongwa mbalimbali hasa Bara la Asia ambako kwa Data za karibuni wamebaki 2700 tu.....Maadui wakubwa wa faru ni BINADAMU MAJANGILI na Simba ambao huwinda watoto wao kwa ajili ya kitoweo.  Kutoweka kwa Faru kumewafanya wawekewe ulinzi wa masaa 24 na askari wa wanyama pori (Park rangers ) 

Pembe hizo zimetengenezwa kwa keratini, protini, sawa na ile inayopatikana kwenye nywele na kucha. 

Yasemekana pia kwamba pembe hizi hutumika kutengenezea sime/dagger pamoja na dawa maarufu ambayo hutumiwa  kuleta heshima nyumbani (VIAGRA) wakafikiri kuwa nguvu zake zinatoka kwenye hiyo PEMBE kutokana na kutumia zaidi ya dakika 40 wakati wa kujamiana, kitu ambacho kimethibitishwa na wanasayansi kwamba si kweli. Kwa nchi za Kiarabau hususan Yemen,  mwanaume huonekana tajiri na mwenye hadhi pale anapokuwa anamiliki sime iliyotengenezwa kwa maligafi ya Faru.

Mwaka 2012 pembe ya Faru ilikuwa ikiuzwa dola 60,000 kwa kilo (Takribani milioni 130 za madafu)  kwenye soko la Dunia. 

Faru wana uwezo mkubwa wa kusikia na kunusa, lakini uoni wao si mzuri sana........Pia Hawana kumbukumbu imara kama Tembo hivyo hawezi kulipiza kisasi.

Anabeba ujauzito wake kwa kipindi cha miezi 18 na huwa anazaa mtoto mmoja ( Mapacha huwa ni nadra). Faru pia ni miongoni mwa wanyama wakubwa wanaopatikana nchi kavu ambapo anaweza kufikia hadi uzito wa 2000-2300KG kwa white rhino na 800-1500KG kwa black rhino. 

Na tofauti kati ya Black rhino na White rhino ni kuwa ana mdomo mweusi uliochongoka ambao unamwezesha kula majani ya juu katika matawi ya mti (Browser) na white rhino yeye anakuwa na mdomo mpana mweupe kwa ndani ambao unamwezesha kula nyasi (Grazers), tofauti nyingine ni kwamba White rhino akiwa na mtoto huwa anatabia ya kumtanguliza mtoto mbele Kama wafanyavyo wamama wa kizungu ambao humbeba mtoto kwa mbele na kwa upande wa Black rhino yeye huwa mtoto anakaa nyuma ya mama kama wafanyavyo wamama wa kiafrica ambao huwabeba watoto wao mgongoni.
 Faru wote wana rangi ya kijivu (Grey colour ) ingawa wakati mwingine huweza kubadilika kutokana na tabia ya kufanya wallowing ( kujiwekea vumbi na matope ili kupunguza joto katika miili yao kwa sababu hawa ni hairless mammals wanyama ambao hawana nywele ) ndio maana wakati mwingine unaweza kuta rangi zao kama zina utofauti fulani.

Kwa hapa Tanzania sehemu nzuri ya kuwaona hawa FARU ni NGORONGORO CRATER. Ni raha sana kumtazama Faru japo ana sura ya kuogofya. 

Ni vyema tu kukumbushana kwamba si rahisi sana kuthamini hazina uliyonayo hadi inapotoweka, ikiwa wengi tulitumia simu zetu kuchukua tukioa la kupatwa kwa jua, habari gani kama utatembelea mbuga ukapiga picha wanyama kwa simu YAKO (Kanuni ya mbugani unatakiwa kuchukua PICHA tu na unatakiw kuacha nyayo tu......TAKE ONLY PHOTOS AND LEAVE ONLY FOOTPRINT......)

ZITAFIKA NYAKATI WANYAMA KAMA HAWA TUTAWAONA AMA KUWASIMULIA KWA PICHA TU .........................yuko mtalii nilikutana naye akaniambia ni mara ya NNE anakuja kuona FARU tuuuuuuu

​By Geofrey Chambua toka vyanzo mbalimbali 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Makala ikhusuyo 'Moringa plant' wameibanduwa, sijuwi hii ya Faru nayo. Ila usikate tamaa endelea kutuelimisha muandishi wa makala hizi Geofrey Chambua toka vyanzo mbali mbali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...