Na Mwandishi wetu, Mwanza
Zaidi ya kampuni 35,000 ziko katika hatari ya kufutiwa leseni na wahusika kufikishwa mahakamani kwa kutofuata sheria za uendeshaji biashara hapa nchini.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajili wa leseni na biashara (BRELA), Bw. Frank Kanyusi amesema jijini hapa kuwa baada ya miezi mitatu kuanzia sasa zoezi hilo litaanza.

“Tunatoa kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa kwa wamiliki wa kampuni kuhakikisha kuwa wanakamilisha taratibu za uendeshaji wa kampuni zao,” alisema.
Alitoa wito kwa makampuni yote nchini kuwasilisha taarifa za kampuni zao kila mwaka pamoja na nakala ya mkaguzi wa fedha na kwamba kutofanya hivyo kutapelekea kufungwa kwa kampuni na kufikishwa mahakani kwa kukiuka sheria.

“Zaidi ya kampuni elfu 35 zitafutwa na kufunguliwa kesi kwa kutotii sheria na kanuni za uwasilishaji wa taarifa za kampuni kila mwaka (annual return),” Bw.Kanyusi aliwaambia waandishi wa habari wakati wa zoezi la usajili wa majina ya biashara na makampuni la papo kwa papo lililoendelea mkoani hapa.

Aliwataka wafanyabiashara na wajasiriamali nchini kutumia fursa ya uwepo wake kurasimisha biashara zao ili serikali iwatambue na kutoa ushirikiano katika kufanya biashara.

“zoezi hili ni endelevu kwa nchini nzima katika kuhamasisha wananchi kurasimisha biashara zao ili wapate urahisiwa kufanya biashara,” alisema Bw.kanyusi jana.

Kwa mujibu wake, mwitikio wa watu katika zoezi hilo ni mkubwa kwani wameweza kusajili majina ya biashara 150 na makampuni 100 kwa siku sita kutokana na semina elekezi iliyotolewa kuhusu umuhimu wa kurasimisha biashara.

Alisema wakala unatambua changamoto iliyopo ya upatikanaji wa elimu ya huduma wanazotoa na ndio sababu wameanza ziara ya kutembea mikoa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma za Brela na umuhimu wa kurasmisha biashara.

Alifafanua kuwa kwa sasa vyombo vya fedha vinaweza kupata taarifa za uhalali wa biashara ya mteja anayetaka kufungua akaunti kupitia mtandao wa BRELA.

“Hii itasaidia kuboresha mazingira ya biashara nchini kwani itampa nafuu mteja muda wa kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo,” alisema Bw. Kanyusi.

Alisisitiza kuwa BRELA itazindua mfumo wa usajili wa kampuni mwezi wa Tatu mwakani ambao utahusisha taasisi nyingine za serikali kama Mamlaka ya Mapato (TRA) ili kurahisha urasimishaji wa kampuni ikiwa ni jitihada za serikali katika kuweka mazingira bora ya biashara nchini.

Alifafanua kuwa mteja atakapo wasilisha maombi ya kufungua kampuni, mfumo utamuunganisha na TRA kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) kwa muda mfupi na mteja atakuwa amekamilisha taratibu na kuendelea na biashara.

Mmoja wa wajasiriamali aliyejitokeza, Bw. Gerald Malamba aliwataka wajasiriamali wenzake kurasimisha biashara zao ili kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara na pia serikali kuweza kutambua walipa kodi wake.

Mjasiriamali, Anitha Samson alisema ni faraja kwake kwa Brela kufika Mwanza kwani wamepata elimu juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara na kutoa wito kwa wakala kufungua ofisi za kanda ili kutoa huduma kwa ufanishi zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...