Na Ally Daud-MAELEZO.

WATANZANIA zaidi ya asilimia 70 wamepewa kipaumbele kushiriki katika shughuli za kujenga uchumi wa nchi kufikia uchumi wa kati katika kutekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi mpaka kufikia mwaka 2020.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa wakati wa ufunguzi wa ripoti ya Tathimini ya Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tunataka kufikia 2020 watanzania asilimia zaidi ya 70 waweze kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kufikia katika uchumi wa kati ili kutekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini” amesema Bi. Issa.

Aidha Bi.Issa amesema kuwa watanzania wanatakiwa washiriki katika shughuli za kiuchumi na wasitegemee zaidi wawekezaji kutoka nje ili kuifanya Tanzania iendelee kiuchumi kutoka ngazi ya mmojammoja hadi kufikia maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Meneja wa Utafiti na ufatiliaji wa Sera hiyo kutoka NEEC Bi. Frola Kajela amesema kuwa Serikali imeandaa sera hiyo ili kuwezesha watanzania kutumia rasilimiali zilizopo katika kuinua uchumi wa nchi na kuweza kumilikiwa na watanzania wenyewe.

“Sera hii inalenga zaidi kwa watanzania kumiliki uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini ili kujishughulisha katika kuleta maendeleo ya nchi kwa jamii na taifa kwa ujumla mpaka kufikia 2020” alisema Bi. Kajela.

Aidha Bi. Kajela amesema kuwa sera hiyo inafanyiwa maboresho ili kuweza kuwafikia watanzania wote katika kuelewa na kumiliki uchumi kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza mpango wa serikali uliyowekwa kuhakikisha watanzania wanajiinua kiuchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...