Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na Wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu kabla ya kufungua Mkutano wa siku mbili wa wajumbe hao unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Balozi Simba aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kuweka mikakati imara ya kupambana na uhalifu huo wa usafirishaji wa binadamu ambapo Tanzania ni mojawapo kati ya nchi zilizoathirika na tatizo hilo. Kulia meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vicent Magere, na kushoto ni Katibu wa Sekretarieti kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Vicent Magere akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) kufungua mkutano wa kamati hiyo wenye lengo la kujadili pamoja na kuweka mkakati wa kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...