Na, Nasra Mwangamilo

Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa yatakiwa kuongeza fursa itakayoziwezesha Serikali za Mitaa nchini kupata fedha za kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hasa katika miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene alipokuwa akizindua rasmi Bodi hiyo leo mjini Dodoma.

“Natambua kuwa nyenzo muhimu za kutekeleza majukumu ya Bodi ni rasilimali fedha ambazo zinatakiwa zipatikane kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo vimeainishwa kwa mujibu wa sheria, kifungu cha 62 cha Sheria ya Bodi ya mikopo kinataja njia mbalimbali ikiwemo kupata fedha kama zitavyoainishwa na Bunge kwa madhumuni ya kuendesha shughuli za Bodi”.Aalisema Mh. Simbachawene.

Aidha alisisitiza kuwa Bodi hiyo ijitahidi kusimamia kwa ukaribu zaidi uwekezaji kwa kuelekeza rasilimali kwenye vitega uchumi vyenye faida kubwa ikiwa ni njia mojawapo ya kujiongezea mapato huku ikiwa na lengo la kuhakikisha inatoa mikopo kulingana na makubaliano baina ya Bodi na Halmashauri husika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene akikata utepe wa nyaraka muhimu zinazohusu Bodi, katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene kwenye picha ya pamoja na wajumbe  wa bodi ya mikopo na baadhi ya watumishi wa bodi hiyo katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...