Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata) kimeiangukia serikali kwa kuiomba iruhusu wenye mabaa kufanya biashara zao wakati wote ili kusaidia kupata fedha za kulipa kodi na mishahara ya wafanyakazi wao.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ali Huseein wakati akizungumza na mtandao wa www.habarizajamii.com Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu changamoto waliyonao wenye mabaa katika kufanya biashara yao hiyo ya uuzaji wa vileo na vinywaji baridi."Tunaiomba serikali kuangalia kwa karibu kuhusu muda wa kufungua baa kwani muda huu wa sasa wa kufungua saa 10 jioni na kufunga saa tano ni mdogo ukilinganisha na ilipokuwa awali wa kufungua wakati wote" alisema Hussein.

Hussein alisema nia ya serikali haikuwa mbaya ya kufungua baa saa 10 lakini hawakuangalia upande wa pili wa wamiliki wa baa hizo kwani wengi wao katika muda huo wengi wao hawafanyi kabisa biashara.aliongeza kuwa wafanyabiashara hao wanahitaji kupata muda wa siku nzima wa kufanya biashara zao ili waweze kumudu kupata fedha za kulipa kodi ya serikali na mishahara ya wafanyakazi na wahudumu wa baa ambao ni wengi,hivi sasa wanashindwa kufikia malengo.

Alisema baadhi ya baa zimepunguza wahudumu wake kutokana na kubanwa na muda huo ambapo wahudumu wamekuwa wakiingia jioni tu baada ya muda wa asubuhi kupigwa marufuku na serikali."Wenye mabaa hivi sasa wapo katika changamoto kubwa ya biashara zao tunaiomba serikali kuangalia jambo hilo kwa sura nyingine ili kuinusuru biashara hiyo kuanzia mmiliki wa baa na viwanda vinavyotengeneza bidhaa hiyo na serikali yenyewe kupata kodi yake.

Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa ombi kwa serikali la kuomba kufunguliwa baa muda wote ili kunusuru biashara hiyo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.
Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck. akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...