Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Ileje

MKUU wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude ameongoza kamati ya ulinzi na usalama kwenda kufukia mfereji uliochimbwa na wananchi wa kata ya Bupigu kuchepusha maji kutoka mto Kalembo kwenda mashambani.

DC Mkude amefanya zoezi hilo ikiwa ni siku chache tangu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Janauary Makamba ,kuagiza kusitishwa na kufukiwa kwa mfereji huo.

wakati wa zoezi hilo la ufukiaji Dc Mkude alimuagiza mkurugenzi wa wilaya hiyo Haji Mnasi kupeleka wataalamu wa umwagiliaji kutoa elimu juu ya ujenzi wa Skim ambazo aziathiri Mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wilaya hiyo amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kujichukulia maamuzi wenyewe kwenye vyanzo vya maji na misitu ya Serikali.

Ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Bupigu kuwa wavumilivu kwani serikali hii ni ya Wanyonge hivyo wanafanya mpango wa kuwawezesha kwa namna nyingine kumudu kilimo cha umwagiliaji kupitia Rasilimali walizonazo.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude (kulia) na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Haji Mnasi wakishiriki zoezi la kuziba mfereji uliochimbwa kuchepusha Mto Kalembo na mmoja wa Wakazi wa kata ya Bupigu kijiji cha Bungu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi, akiwa na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo kuziba maji katika eneo lilichimbwa na mmoja wa wakazi wa Kata ya Bupigu kwa lengo la kuchepusha mto Kalembo kwenda kwenye Mashamba .
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje ,Haji Mnasi, akivuta maji yaliyowekwa kuziba mto Kalembo uende sehemu nyingine hali inayohatarisha mazingira katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje ,Joseph Mkude akizungumza jambo na mkurugenzi wa wilaya hiyo Adji Mnasi, juu ya atahari za mfereji huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...