Na.
Immaculate Makilika – MAELEZO.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari– MAELEZO Bw. Hassan Abbas amesema kuwa waandishi wa habari hawapaswi
kuwa na wasiwasi kuhusu muswada wa huduma za habari kwa vile hakuna mwandishi wa
habari atakayefukuzwa au kuachishwa kazi kwa kigezo cha kutokuwa na elimu
katika ngazi ya shahada ya kwanza.
Akizungumza
katika kipindi cha mahojiano cha Clouds360 kinachorushwa na kituo cha
televisheni cha Clouds, Bw. Abbas amesema hakuna haja ya waandishi wa habari kuuhofia
muswada huu badala yake wausome na kuelewa na kisha watoe maoni yao ili
kuuboresha zaidi.
“Sheria
itatoa kipindi cha miaka 5 ili watu wajiendeleze katika taaluma hii ya habari,
hivyo hakuna mwandishi wa habari atakayefukuzwa au kusimamishwa kazi kwasababu
ya huu muswada kwa vile lengo ni kuwaandaa waandishi ili waweze kufanya kazi vizuri
kwa kuzingatia taaluma”alisema Bw. Abbas
Bw.
Abbas aliongeza kuwa kigezo cha taaluma kwa wandishi wa habari hakitaainishwa
katika sheria bali katika kanuni.
Aidha
Bw.Abbas ameongeza kuwa katika historia ya masuala ya habari nchini huu ni muswada
pekee unaolenga kulinda wanahabari kwani unazungumzia hali halisi ya mwandishi wa
habari, ukilinganisha na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 inayozungumzia haki
ya chombo cha habari pekee.
Muswada
wa huduma za habari umetokana na maoni ya wadau baada ya kuona mapungufu katika
sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo ilitungwa wakati ambapo hakukua na maendeleo
makubwa katika sekta ya habarinchini.
Aidha,wadau
na waandishi wa habari pamoja nchini wameombwa kuendelea kutoa maoni yao kwa kutuma
barua pepe kupitia anuani ya cna@bunge.go.tz
ilikutoa fursa ya kuboresha muswada huo kabla ya kuwa sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...