Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ( DED) Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akizungumza juzi katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Albert Msole na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary.Picha na Mary Margwe


Na Mary Margwe, Simanjiro,

Mkurugenzi huyo aliliambia baraza la Madiwani kuwa halmashauri yake inakusudia kupima viwanja vipatavyo 300 katika Mji mdogo wa Mirerani hivi karibu ni,vitakavyowaingizia zaidi ya sh.mil.600.

Wakati huo huo, akiwakilisha mapendekezo ya maazimio ya kikao cha kamati ya fedha, uongozi na Mipango,mwenyekiti wa kamati hiyo, Sendeu Laizer, alisema katika mkakati wa kukusanya mapato ,kamati hiyo imeridhia pendekezo la kubinafsisha vyanzo vya mapato ya kodi ya huduma, ada ya matangazo na uuzaji wa viwanja.

Laizer ambaye ni diwani wa kata ya Orkesumet Wilayani Simanjiro,alisema wakati umefika wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kukaa na mkandarasi wa mradi wa maji Olchoronyori akiwa na vielelezo vyake vyote vinavyoonyesha malipo na kazi alizokwisha zifanya ili kubaini tofauti iliyopo na kama kutakua maelewano kazi hiyo iendelee na kama hakuna muafaka yafanyike mapitio ya mkataba kuona uwezekano wa kuvunja mkataba ili kuona kama atapatikana mkandarasi mwingine atakayemalizia kazi hiyo.

Akiwakilisha mapendekezo ya kamati ya Uchumi, ujenzi na mazingira ,mwenyekiti wa kamati hiyo Loishiye Lesakwi, aliliambia baraza hilo kuwa mkurugenzi mtendaji ahakikishe kuwa anawaandikia barua watendaji wote wa vijiji yenye maelekezo ya namna ya kukusanya michango katika jamii na kuweza kutoa taarifa za mapato na matumizi ya michango hiyo.

Lesakwi, ambaye ni diwani wa kata ya Oljoro namba 5, alisema pia mkurugenzi huyo ahakikishe kuwa minada yote unajua na vyoo pamoja na kufanya usafi kwenye minada yote ambayo halmashauri inakusanya ushuru.

Akisoma mapendekezo ya maazimio ya kikao cha kamati ya kudhibiti Ukimwi kwa niaba ya makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Albert Msole, diwani wa viti maalum Tarafa ya Emboreet,Rehema Naamani, alisema mkurugenzi mtendaji aangalie uwezekano wa kupata afis ustawi wa jamii kwa ajili ya Mji mdogo wa Mirerani,kwa kile alichodai kuwa kuna uhitaji mkubwa wa mtaalam huyo katika eneo hilo.

"Maafis watendaji wa kata waandikiwe barua ya kuwataka kuwasilisha kwa mkurugenzi huyo majina ya wanafunzi wa sekondari wanaoishi katika mazingira hatarishi, kazi hiyo if any we kwa kushirikiana na wakuu wa sekondari wote" alisema Naamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...