Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” ameahidi kujenga uwanja wa michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini.

Akizungumza katika Mahafali ya Nane ya shule hiyo, Jokate alisema kuwa ameguswa na changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.Tayari Jokate amekabidhi viwanja vya netiboli na mpira wa kikapu kwa shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.

Jokate ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, alisema kuwa serikali peke yake haitaweza kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu na nyinginezo na hivyo inahitaji msaada kutoka kwa sekta binafasi na wadau.

“Nashukuru kwa kunichagua kuwa mgeni rasmi katika mahafali haya, hii imenipa faraja kubwa sana, nimesikia changamoto mbalimbali, kwa kuanzia nitaanza kujenga uwanja wa michezo na matundu ya vyoo,” alisema Jokate.

Alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.
Jokate Mwegelo akimkimkabidhi zawadi ya kuwa mwanamichezo bora wa wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.

Jokate Mwegelo akimkimkabidhi zawadi mwanafunzi mwenye nidhamu bora kwa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.

Jokate Mwegelo akiserebuka na wanamuziki wa bongo fleva wanaosoma katika shule ya sekondari ya Majani ya Chai wakati wa Mahafali ya Nane yaliyofanyika juzi. Jokate ameahidi kuijengea shule hiyo uwanja wa michezo na matundu ya vyoo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...