Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu,Mkoani Manyara,Hudson Stanlay Kamoga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusiana na mikakati aliyojiwekea katika utendaji wake wa kazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo..Picha na Mary Margwe.


Na Mary Margwe, Mbulu

.Ndoto yake ni kuibadilisha Mbulu kuwa nchi ya vitunguu swaumu.(Mbulu the land of garlic).Asisitiza mambo muhimu matatu ya kuleta mabadiliko ya maendeleo yanayotokana na neno P I A

P---Patriotism---Uzalendo
I----Integrity. ----Uadirifu na
A---Accountabiliyt---Uwajibikaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini,Mkoani Manyara , Hudson Stanley Kamoga, amewataka watendaji,madiwani na wananchi kwa ujumla kumpa ushirikiano katika utendaji wake wa kazi ya kuwatumikia wananchi Wilayani humo kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo.

Akiongea na waandishi wa habari Jana ofisini kwake, Kamoga alisema ushirikiano katika nyanja yoyote ile inahitajika ili kufikia malengo,hivyo naye anaomba apewe ushirikiano ili kuweza kufikia malengo aliyojiwekea katika kuhakikisha Mbulu unajua na maendeleo ya kweli na si vinginevyo.

Kamoga alisema ushirikiano huo uende sambamba na kuwataka wakuu wa idara kumpa mpango kazi wake wa mwezi mmoja kuwa mini amefanya kwenye idara yake, kama idara wamekutana na vikwazo / changamoto gani na ni kwa namna gani wamejipanga kukabiliana na changamoto hizo

Kamoga alisema yeye kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbulu, angependa kuona madiwani na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo wakiwa wanazungumza lugha moja tu ya maendeleo na si vinginevyo.

"Lazima kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu,nihakikishe watendaji na madiwani wanafanya kazi kama timu moja, kwani siku zote umoja ndio hujenga kitu chochote cha maendeleo na msingi wa maendeleo ni ushirikiano yaani umoja,hivyo uwezo ninao wa kulisimamia hili na hatimaye kuweza kuona tuko wapi, tumetoka wapi na tunatarajia kwenda wapi " alisema Kamoga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunakuombea sana Mkuruguenzi Mungu akufanikishe na watu wa Mbulu wote. Pastor George -Daressalaam!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...