Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MKUFUNZI na mjumbe wa baraza la Taifa la Usalama Barabarani Nchini, Henry Tandau amewaasa madereva kufuata sheria pale wanapokuwa barabarani, kwani madereva wasiofuata sheria wanachangia asilimia kubwa ya ajali zinazotokea na kusababisha vifo.

Tandau amesema hayo wakati wa semina elekezi ya wanahabari ya namana ya kuandika na kuripoti habari za usalama barabarani inayoratibiwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Nchini ( TAMWA) pamoja na taasisi zingine.

"Makosa mengi yanayosababisha ajali ni kutokana na madereva kushindwa au kudharau sheria kama zilivyoelekeza, matokeo yake hupelekea  kuleta maafa kwa jamii hasa baada ya ajali kutokea  pamoja na ulemavu", amesema Bantu.

Sheria namba 30 ya Usalama Barabarani iliyounda Baraza la Usalama Barabarani limekuwa na mapungufu mengi sana huku ikiwa haijaweka wazi sheria madhubuti ya kuhakikisha wanakuwa na nguvu kuwabana madereva pindi wanapofanya makosa huku elimu isiyo toshelezi ni chanzo kikubwa cha ajali kutokea na kusababisha vifo na ulemavu kwa jamii.

Katika njia bora ya udereva, Bantu amesema udereva wa kujihami, fizikia ya dereva na saikolojia ya dereva ni msingi mkubwa unaoweza kuleta manufaa katika jamii kwani atakuwa anaendesha gari kwa umakini na kabla ya kufanya maamuzi ataangalia, atakijadili na kisha kufanya maamuzi.

Dereva mzuri ni yule kabla ya safari hulikagua gari yake na kuhakikisha iko sawa kwa safari kuanzia ndani mpaka nje na pia matumizi sahihi ya matairi kulingana na aina ya sehemu unayoelekea pamoja na mzigo utakaoubeba au uwezo wa gari utaweza kukufikisha safari yako unapokwenda. 
Mkufunzi na mjumbe wa Baraza la Usalama Barabarani Nchini Henry Bantu akielezea jambo mbele ya wanahabari waliohudhuria semina elekezi ya masuala ya Usalama Barabarani na jinsi ya kuandika matukio hayo.

Baadhi ya Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumibi humo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...