Na Bashir Yakub.
Ni vema kujua nani anapaswa kupewa kipaumbele cha kusimamia mirathi pale mwenye mali anapokuwa ameaga dunia. Mara kadhaa mjadala huibuka baina ya wanafamilia hasa pale inapotokea kuwa marehemu alikuwa na mke zaidi ya mmoja na kila upande kuna watoto.
Lakini pia hata pale marehemu anapokuwa na mke mmoja mjadala huu napo waweza kuibuka kati ya wanaotegemewa kurithi juu ya nani awe msimamia mirathi. Hii si pale tu anapokufa baba lakini pia hata panapo mswiba wa mama mjadala huu huibuka.
1.WOSIA KUTAJA MSIMAMIA MIRATHI.
Ikiwa marehemu ameacha wosia na katika wosia huo imeelezwa wazi nani atakuwa msimamizi wa mirathi basi huyo aliyetajwa ndiye atakuwa msimamizi wa mirathi . Wosia unaweza kumtaja mtu mmoja kusimamia mirathi au zaidi ya mtu mmoja. Kwa vyovyote utakavyotaja hao waliotajwa ndio watasimamia mirathi.
2. WOSIA KUTOTAJA MSIMAMIA MIRATHI.
Si wakati wote wosia hutaja msimamia mirathi. Hii yaweza kutokea kwa kutokujua kwa aliyeandika wosia au kujua lakini kuacha makusudi kwasababu nzuri anazozijua mwenyewe. Kwa namna yoyote itakavyokuwa wosia usipotaja nani asimamie mirathi basi ni wajibu wa wanafamilia kuhakikisha anapatikana msimamizi ili agawe mali kutokana na wosia unavyoeleza.
Muhimu ni kuwa ni lazima apatikane msimamizi wa mirathi. Aweza kuwa mmoja au zaidi. Swali kwetu ni ikiwa kumetokea mgogoro kuhusu nani asimamie mirathi je nani afaa zaidi kuliko wenzake kupewa kipaumbele kwa mujibu wa sheria.
3.NANI APEWE KIPAUMBELE CHA KUSIMAMIA MIRATHI KATI YA WARITHI WA MAREHEMU.
Sura ya 352 ya sheria ya usimamizi mirathi ndiyo huongoza jambo hili. Ikumbukwe tumesema hapo juu kuwa suala la nani apewe kipaumbele cha kusimamia mirathi linaibuka pale tu ambapo marehemu hakuacha wosia kabisa au ameacha wosia lakini ndani mwake hakumtaja msimamizi wa mirathi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...