Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam ambapo Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wajasiriamali kuwafichua watendaji wa mamlaka za kurasimisha biashara watakaowadai rushwa wakati wa kupatiwa huduma ya kurasimisha biashira zao.

Makamu wa Rais alitoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati kufungua Kongamano la Pili la Sauti ya Wanawake Wajasirimali Tanzania (VoWET).Alisema wanawake hawapaswi kuogopa kuwafichua watendaji wanaowaomba rushwa kwani wanawakwamisha katika harakati zao (wanawake) za kujiendeleza kibiashara,kiuchumi na pia kukwamisha juhudi za serikali katika kuinua maendeleo ya Wanawake nchini.
Rais wa VoWET Bi. Maida Waziri (kulia) akihutubia wakati wa Kongamano la Pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania ambapo licha ya kupongeza jitihada za serikali ya awamu ya tano katika masuala mbali mbali ya kumuwezesha mwanamke pia alielezea changamoto ambazo wanawake wanakutana nazo katika shughuli zao za kuwainua kiuchumi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya kazi za ubunifu zilizofanywa na Wanawake Wajasiriamali kabla ya ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...