Afisa masoko Platinum Credit Tanzania, Gideon Lufunyo (kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji ambayo ni sawa na tani 15 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu ikiwa ni msaada wa taasisi hiyo kwa waathirika wa tetemekonla Ardhi mkoani humo.
Kampuni ya Platnum Credit Tanzania Leo imekabidhi msaada wa mifuko 300 ya sumenti kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani humo.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo leo, Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo,Gideon Lufunyo
alisema tetemeko hilo limeleta madhara
makubwa ambayo yamewagusa na kuamua kusaidia serikali katika kurejesha miundombinu yake hasa katika mshule katika hali nzuri ili masomo yaendelee na watoto wapate elimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...