Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa ameshika kibao alichoweka alama ya kiganja chake, kuunga mkono umoja na mshikamano wa nchi za Kiafrika zinazohusiana kiuchumi na Korea Kusini baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Tano wa ushirikiano huo kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC) katika ukumbi wa Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (Katikati) (Kulia kwake) na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Akinwumi Adesina, (Kushoto) Baada ya kufunguliwa Rasmi kwa Mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Kiafrika, unaofanyika Mjini Seoul, Korea Kusini
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa na Maafisa kutoka Tanzania, wakitoka kwenye Ukumbi wa Mikutano  wa Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini, baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika, mjini Seoul, Korea.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Mpango (Mb), akipokea zawadi ya kitabu kinachoelezea njia zilizotumiwa na nchi ya Korea Kusini, kupiha hatua kubwa ya maendeleo, kutoka kwa Afisa Mikopo wa Benki ya Exim ya Korea Kusini, Park Gil Jong, kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa tano wa ushirikiano wa Korea Kusini na nchi za Afrika  (KOAFEC), Mjini Seoul, Korea Kusini. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...