MBUNGE wa viti maalum CCM  mkoa wa Iringa, Rose Tweve ametembelea kikundi cha akina mama wa kata ya Maduma Wilaya ya Mufindi na kuwapongeza kwa juhudi zao wanazozifanya katika shughuli za ujasiriamali.

Tweve akiwa katika kata hiyo aliweza kuwapatia wakina mama hao pesa taslimu milioni moja kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kibiashara na kuacha kuwa tegemezi .

Akizungumza na wakina mama hao, Tweve ameweka wazi mpango wake wa kuwasaidia wanawake wote wanaoanzisha vikoba au vikundi kwa ajili ya ujasiriamali zaidi wajitume zaidi kuhakikisha wanakuza mitaji yao.

Katika ziara hiyo, Mbunge huyo aliongoza na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Mufindi na wao waliweza kuchangia Laki tano kwa wakina mama hao.

Tweve amesema kuwa wakati wa kampeni za mwaka jana pamoja na ilani ya chama cha Mapinduzi aliwaahidi wakina mama wa Iringa kuwa ataungana nao katika kuwasaidia kujiinua kiuchumi na kupambana na umaskini kwa Kuanzisha mfuko wa wanawake ambao umeshaanza kufanya kazi.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Rose Tweve akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa akina mama hao wa Maduma alipoenda kuwatembelea na kuangalia namna wanavyojishughulisha katika biashara zao za ujasiriamali.
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve akimkabidhi moja ya akina mama wa Maduma fedha taslimu kiasi cha milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mitaji yao ya biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...