NA VICTOR MASANGU, RUFIJI.
BAADHI ya wakinamama wajawazito wanaoishi katika vijiji vya Mbunju na Mbambe vilivyopo kata ya Mkongo. Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya kujifungulia wakiwa njiani kutokana na kuwepo kwa umbali mrefu kutoka makazi wanayoishi hadi kufika katika zahanati au kituo cha afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Wakinamama hao wametoa kilio chao wakati walipotembelewa na mbunge wa jimbo la Rufiji ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wake pamoja na kero zao ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ya kuleta chachu ya maendeleo.
Zarau Kiambwe Tabia Athumani,pamoja na Suzan Masela ni miongoni mwa wakinamama hao wanaokabiliwa na changamoto hiyo,walisema wakati mwingine wanapata wakati mgumu hususan nyakati za usiku kutokana na kukosa usafiri hivyo kuwalazimu kujifungulia njiani hali ambayo inahatarisha uhai wa kupopteza maisha yao ukizingatia na gharama za usafiri wa piki piki ni kubwa hivyo wanashindwa kuzimudu kutoka na kutokuwa na kipato chochote.
Aidha wakinamama hao wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo la Rufiji kwa kushirikianana serikali ya awamu ya tano kuliingilia kati suala hilo ili kuweza kuwasaidia wananchi kwa kuwajengeaa zahanati pamoja na vituo vya afya vilivyvyo karibu na maeneo wanayoishi ili kuweza kupata huduma ya matibatu kwa urahisi bila ya usumbufu.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mbunju na Mbambe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuwatembelea kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na baadhi ya wanakijiji hicho kwa ajili ya kuweza kujadili kero zinazowakabili.
Mbunge wa Rufiji akifurahia jambo baada ya mzee maarufu kijijini hapo kumpa pongezi za dhati kwa kuhudi zake anazozifanya katika kuwataumikia wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na baadhi ya wanakijiji hicho kwa ajili ya kuweza kujadili kero zinazowakabili.
Mbunge wa Rufiji akifurahia jambo baada ya mzee maarufu kijijini hapo kumpa pongezi za dhati kwa kuhudi zake anazozifanya katika kuwataumikia wananchi wa jimbo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...