Na Kijakazi Abdalla, 
Maelezo - ZANZIBAR
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetumia kiasi ya dola 90 elfu kuifanyia matengenezo ya kawaida Meli ya MV Mapinduzi ll iliyopelekwa Chelezoni Mombasa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji  Mustafa Aboud Jumbe mara baada ya kuwasili Bandarini Malindi amesema itaanza safari zake za kawaida za Pemba kuanzia kesho ili kupunguza usumbufu wa usafiri uliojitokeza baada ya kuondoaka meli hiyo. 
Alisema kuwa meli hiyo imefanyiwa matengenezo ya kawaida  na hakuna kitu kilicho badilishwa na baada ya  matengenezo hayo itakuwa  chini ya Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwa udhamini wa mtengenezaji.
Hata hivyo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji  amesema hivi sasa Serikali imo katika mchakato wa kununua meli nyengine mbili mpya, moja  kwa ajili ya abiria na mizigo na nyengine itakuwa ya mafuta.
Mapema Nahodha wa Meli hiyo Abdulrahman  Mzee amesema matengenezo ya meli yaliyofanyika yamekwenda sambamba na muda uliopangwa na  yamefanywa kwa hali ya ubora kabisa.
Amesema kuwa kufanyika kwa matengenezo ya meli hiyo ni jambo la kawaida kwa chombo chochote cha usafiri jambo linalokipa ubora chombo husika.
Meli ya MV Mapinduzi ll iliondoka Zanzibar  wiki mbili zilizopita kwenda chelezoni  Mombasa na imerejea  Zanzibar leo kupitia  Pemba ikiwa imechukua  abiria 1200 pamoja na mizigo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...