Mfalme Mohammed  VI wa Morocco akibusu Masahaf kabla ya kumkabidhi Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti kwenye eneo la BAKWATA Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016.  Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abukary Zubeir. Jumla ya Masahaf 10000 zilikabidhiwa na Mfalme huyo
 Mfalme Mohammed  VI wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016
 Mfalme Mohammed  VI wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016
Mfalme   Mohammed VI wa Morocco,  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Rais Mstaafu Alhaj  Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Bilal wakiwa katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa msiki uliofnywa na Mfalme Mohammed wa Morocco kwenye  eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salam Oktoba 25, 2016.  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Masha Allah!. Jazaqallahu Khayr kwa yote aliyoyakubali kutukidhia Mfalme Mohammed VI wa Morocco, khusuana na hilo la ujenzi wa Masjid (Mskiti), basi In Sha Allah, jaza yake ataikuta kesho huko usoni twendako. Hakika mambo mithli ya hayo ndizo hizo 'Swadaqatin'jariya' tuhimizwazo kujitolea endapo hali na uwezo vinarukhusu. Kadhalika nimshkuru na kumpongeza kwa dhati Mh. Rais wetu Mh. John Pombe Joseph MAGUFULI kwa jitihada zake za dhati na za kipekee kabisa katika kuhakikisha watanzania wana kila sababu ya kupata maendeleo ya kila hali nchini katika nyanja zote za kimaisha pasina kujali wala kubaguwa tofauti zozote zile, ima za kidini, kikabila, rangi ,kisiasa, kiitikadi n.k. Kwa kweli amekuwa msatari wa mbele kwa hali na mali na hata kama ni kwa kujitolea muhanga, almuradi kuhakikisha kujengeka kwa Tanzania mpya itakayoongozwa na gurudumu la maendeleo ya kiuchumi khususan katika uchumi huu wa viwanda ambao utaambatana na maendeleo takriban katika kila sekta nchini. Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake. Ibariki Afirka na Dunia kwa jumla.

    ReplyDelete
  2. Kabla hajaondoka jamani muombeni ajenge chuo Kikuu kikubwa huko kanda ya ziwa woote tumebanana Udom nna UDSM . Tutakuwa tumeweka balance ya nguvu . Elimu dunia ni ufunguo wa maisha .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...