Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa akisikiliza Changamoto mbalimbali walizonazo baada ya kufanya ziara katika wilaya ya Longido,jijini Arusha.

Mkurugenzi halmashauri ya Longido bwana Juma Mohamed Muhina ameamuru kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi mtendaji wa kata ya Egirai Lumbwa Wilayani Londigo bwana Paulo Luka kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Natroni Flamingo.

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wananchi wa kijiji cha Meligoi kata ya Egirai Lumbwa kuikata taarifa iliyosomwa na mtendaji wa kata hiyo iliyoonyesha ujenzi mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha milioni 50 lakini michango ya awali ilikuwa milioni 12 na kati ya hiyo milioni 4 tu ndio ilikuwa michango ya wananchi.

Wananchi hao walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa akisikiliza Changamoto mbalimbali walizonazo baada yakufanya ziara katika kijiji hicho , walisema kuwa wao wanavyojua wamechanga zaidi ya fedha zilizotajwa kwenye taarifa hiyo.

Hivyo Gambo alimtaka Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri kufafanua juu ya matumizi ya fedha hizo, akifafanua Bi. Mwajuma mdaira alisema alifanya ukaguzi na kugundua kuwa fedha zilizokusanywa kwa njia ya michango ilikuwa milioni 95 na milioni 50 kati ya hizo zilitumika kwenye marekebisho ya majengo ya shule japo hakukuwa na mikata yoyote iliyoingiwa kati ya shule na mkandarasi.

Pia fedha hizo zilitumika bila kutumia stakabadhi za malipo za halmashauri, na kuna wawekezaji 2 ambao ni Winget Windros Safari walichangia mifuko 200 ya simenti na mingine 200 ilitolewa na Kilomberong Hunting kusaidia ujenzi lakini mifuko 144 kati ya hiyo iliuzwa na fedha zake hazikujulika matumizi yake lakini bado anaendelea na ukaguzi zaidi.

Hivyo kumpelekea Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kutaka kufahamu hatma ya mtendaji huyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri aliyekili kupata taarifa hiyo jana yake tu na hapo hapo akamuamuru kamanda wa polisi Wilaya kumkamata mtendaji huyo nakumpeleka kituoni kwa maelezo na upelelezi zaidi juu ya ubadhilifu huo.
Badhi ya wananchi wa kijiji cha Meligoi walioikata taarifa ya mtendaji wa kata yao, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo(hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara, kijiji hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...