Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akihojiwa na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, kuhusiana na sakata la Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza kugoma kukabidhi mihuri yao ya utendaji kazi.


Na George Binagi-GB Pazzo

"Hii mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni dili, hivyo haitambuliki kwa sasa, kwanza imesababisha migogoro mingi kwa wananchi ikiwemo uuzaji wa viwanja kiholela". Amesisitiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba.Ameshikilia msimamo wake kwamba mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza haitambuliki kama awali alivyosema kwamba waikabidhi ofisini kwake.

Leo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutorudisha mihuri hiyo huku wakitishia kutoshirikiana na Watendaji Jijini Mwanza.Juzi jumamosi Wenyeviti 174 wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza, walivunja kikao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, baada ya Mkurugenzi huyo kuwataka kukabidhi mihuri yao.

#Lakefm #BinagiBlog #BMG #Mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...