Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam 
SERIKALI imesema hakutokuwa na matumizi mabaya ya mamlaka anayopewa Waziri anayesimamia tasnia ya habari katika muswada wa sheria ya huduma ya habari isipokuwa kwa masuala yatakayohatarisha usalama wa Taifa.
Imesema Serikali haiwazuii waandishi wa habari kukosoa sera, matamko na ahadi mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wa kitaifa pindi wanaposhindwa kutekeleza maagizo wanayoyatoa kwa wananchi.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Hassan Abbas alisema muswada huo unatoa fursa kwa chombo cha habari kupeleka malalamiko yake mahakamani pindi inapotokea kutokubaliana na hatua itakayoweza kuchuliwa na Waziri mwenye dhamana ya habari.
Kwa mujibu wa Abbasi alisema yapo masuala kadhaa yanayopaswa kuchuliwa hatua za haraka za maamuzi ikiwemo suala la uchochezi, uasi wa kikundi fulani cha watu kinachotaka kuigombanisha Serikali na wananchi.
Aliongeza kuwa hata katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.


Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha CLOUD wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam na kuelezea maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria ya huduma ya Habari. Wengine ni Watangazaji wa Kituo hicho, Babbie Kabae (kushoto) na Hassan Ngoma. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam, Rehure Nyaulawa akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas kuhusu utendaji kazi wa gari la urushaji matangazo ya nje. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari. 
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Uhariri ya Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari. (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA) .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...