Na Theresia Mwami TEMESA TANGA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka wafanyakazi wa kivuko cha Mv Tanga kuzingatia usalama wa abiria kwa kufata kanuni na Sheria za usafirishaji wa abiria kupitia vivuko.

Amesema hayo alipotembelea na kuongea na watumishi wa kivuko cha MV. Tanga kinachosafiri kati ya Pangani na Bweni na kuwasisitiza watumishi hao juu ya suala la usalama wa abiria na kuwa waaminifu katika ukusanyaji wa mapato ya kivuko hicho.

Ndugu zangu hapa tunabeba roho za watanzania wenzetu tuwe makini sana na kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo ili kuhakikisha usalama wa hawa abiria tunaowahudumia” Alisisitiza Dkt Mgwatu.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma amemuahakikishaia Mtendaji Mkuu kuwa watazingatia taratibu na Sheria zilizopo ili kuhakikaisha usalama wa abiria wanaowahudumi kupitia kivuko cha Mv Tanga na vivuko vingine vilivyopo mkoani Tanga.

Aidha kwa upande wao watumishi wa Mv Tanga wamemwaomba Mtendaji Mkuu kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizopo zikiwepo uhaba wa vifaa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huyo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma (kushoto) alipotembelea kituo hicho, kulia ni Mhasibu wa TEMESA Tanga Bw. Lusenga David. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto aliyesimama) akizungumza na watumishi wa TEMESA Tanga wakati alipotembelea kituo hicho kuangalia hali ya utendaji kazi, kulia ni Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma.
Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Tanga 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...