Na Veronica Simba

Mwekezaji mzalendo katika Sekta ya Madini nchini, Aloyce Msabi, amechangia mifuko 400 ya saruji yenye thamani ya shilingi 4,800,000 kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu mkoani Kagera.

Akikabidhi hati ya malipo husika (Bank Slip) aliyoyafanya katika Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe kwenye akaunti ya ‘KAMATI YA MAAFA KAGERA,’ kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo; Msabi alisema ameamua kuitikia wito wa Serikali kusaidia wahanga hao ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa umma kile anachopata kutokana na uwekezaji wake katika sekta ya madini.

Pia, aliongeza kuwa, akiwa ni mwananchi mzalendo, ameguswa na janga lililowapata wananchi wa Kagera na hivyo kuamua kuchangia ili kuwasaidia.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu Pallangyo, alimshukuru Msabi kwa niaba ya Serikali kwa moyo wa ukarimu aliouonesha na kutoa rai kwa watanzania wengine, hususan wawekezaji wazalendo kuiga mfano huo na kujenga tabia ya kusaidia jamii zinazowazunguka kutokana na kipato wanachopata kupitia shughuli wanazofanya.

Hati hiyo ya malipo, imewasilishwa kwa Kamati ya Maafa iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.Walioshuhudia makabidhiano ya hati hiyo katika Ofisi za Wizara ni pamoja na Kaimu Kamishna wa Madini –Mhandisi John Shija, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli-James Andilile, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi-Lusius Mwenda na Mratibu wa Idara ya Madini, Phillip Ngereja.

Pamoja na shughuli nyingine mbalimbali katika sekta ya madini; Msabi pia hupata asilimia moja ya uzalishaji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA-North Mara, ambao aliingia nao ubia kupitia leseni yake ya uchimbaji.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto), akipokea hati ya malipo (Bank Slip) kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko Kagera, kutoka kwa Aloyce Msabi (kulia). Wengine pichani kutoka kushoto ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli-James Andilile, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi-Lusius Mwenda na Kaimu Kamishna wa Madini- Mhandisi John Shija.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto), akipokea hati ya malipo (Bank Slip) kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko Kagera, kutoka kwa Aloyce Msabi (kulia). Wengine pichani kutoka kushoto ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli-James Andilile, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi-Lusius Mwenda na Kaimu Kamishna wa Madini- Mhandisi John Shija.
Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli-James Andilile, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi-Lusius Mwenda, Kaimu Kamishna 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...