Ni wiki ya tisa sasa tangu mziki mnene wa efm redio uzinduliwe na jumamosi ya tarehe 29 mwezi wa kumi wakazi wa mlandizi wamefurahishwa vilivyo na muziki mnene wa efm redio kutoka kwa rdjs wa redio hiyo pamoja show za wasanii kutoka kwa doggo nigga, na yuda msaliti pamoja na wasanii wengine chipukizi wa singeli.

Vilevile zawadi kabambe zilitolewa kwa wakazi hao wa mlandizi waliofika katika tamasha hilo kutoka kampuni ya Vodacom ikiwemo simu tatu, t-shirts, kofia, pamoja na muda wa maongezi
Msanii wa muziki wa singeli alimaarufu kwa jina la Yuda Msaliti akiwatumbuiza wakazi wa mlandizi
Baadhi ya sehemu ya watu waliohudhuria tamasha hilo
Droo yakujishindia simu ikichezeshwa kutoka Vodacom wapili kutoka kushoto ni James Kigodi Meneja Masoko akifuatiwa na Meneja masoko na matangazo wa Vodacom Materi Mushi
Dogo niga akiwapagawisha wakazi wa Mlandizi​.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...