Mradi mkubwa wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan, Loliondo umezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki, miaka miwili tangu kutiwa saini kwa uanzishwaji wake kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) na kampuni ya Samsung.
Mganga Mkuu wa Wilaya Ngorongoro, Dk. Omari Sukari akitoa maelezo ya huduma mbalimbali za Afya zitakazokuwa zikipatikana ndani ya moja ya makontena ya kijiji cha Kidigitali cha Samsung (Samsung Digital Village) kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma maalum za afya uliofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Rashid Taka akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto aliyeketi) kuhutubia wageni waalikwa na wanakijiji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Arusha.
Pichani juu na chini ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akisoma hotuba katika hafla ya uzinduzi wa kijiji cha kidigitali chenye kituo cha huduma maalum za afya pamoja na kituo cha elimu kwa njia ya mtandao kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu uliofanyika kwenye kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Hiki kitakuwa ni kijiji cha nne cha digitali barani Afrika cha kwanza kikiwa nchini Afrika Kusini huku kingine kikiwa Gabon na Ethiopia.Kijiji hicho cha digitali ni nadharia ya Samsung katika kurejesha faida kwa umma na kina huduma mbalimbali ambazo zikiunganishwa na haja ya wananchi zitasaidia kubadili maisha ya wamasai na kuondokana na utegemezi wa mifugo pekee.

Uzinduzi rasmi wa kijiji hicho umefanywa na Mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo kwa niaba yaWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu.

Kijiji hicho cha digitali kina shule yenye tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua.

Mradi huo ambao ulishuhudiwa utiaji saini na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Bi. Leah Kihimbi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Dkt. N. Iriya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dar es Salaam na wafanyakazi wa UNESCO mwaka 2014, kukamilika kwake kunawezesha UNESCO na serikali ya Tanzania kuwapatia wakazi wa eneo hilo huduma bora za afya na vijana wa Kimasai nafasi ya kupata elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.

Utiaji saini wake katika mwaka huo ulifanywa na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi Shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo .Kupitia kijiji hicho vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao kutokana na kupatiwa tablet ambazo zitawawezesha kujifunza hata wakiwa nje wakichunga mifugo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...