Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO. Geita 


Shirika la Plan International limetoa rai kwa Serikali kuanzisha Idara ya Kazi katika maeneo ya migodi ili ishirikiane na wachimbaji wa madini kuhakikisha tatizo la ajira kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18 linakoma.

Hayo yamesemwa leo mkoani Geita na Mratibu wa Mradi wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto wa shirika hilo, Maxmillian Kitigwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya changamoto zinazoukabili mradi huo.

Kitigwa amesema kuwa katika Mkoa huo kuna changamoto nyingi zinazowakabili watoto lakini kukosekana kwa Idara ya Kazi katika maeneo ya migodi kunasababisha uvunjwaji mkubwa wa haki za watoto kwa kuwa watoto wengi wanakimbilia kufanya shughuli mbalimbali katika maeneo hayo ili kujipatia kipato.

”Sasa hivi Geita imeshakuwa Mkoa, na mkoa huu umezungukwa na migodi mikubwa hivyo Serikali inatakiwa kuweka Idara ya Kazi katika sehemu hizi ili kuzuia ajira za watoto pamoja na kukomesha unyanyaswaji unaofanywa kwa baadhi ya watu wanaofanya kazi huko”, alisema Kitigwa.
Meneja wa Miradi wa Shirika la Plan International - Geita, Gratian Kweyamba akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya malengo ya Mradi wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto, kulia ni Mratibu wa Mradi huo, Maxmillian Kitigwa. Mradi huu wa miaka mitatu unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa Geita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...