Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ.

Mashindano ya mchezo wa Golf ya PWC Trophy yanayotarajiwa kufanyika leo Jumamosi Oktoba 22 katika uwanja wa Golf wa Lugalo yanatarajiwa kutumika kuchuja Wachezaji wa Timu ya Taifa ya golf wanaotarajia kushiriki mashindano ya East Afrika Challenge nchini Ethiopia.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Jijini Dar es Salaam yatakapofanyika mashindano hayo Brigedia jenerali Michael Luwongo na kuongeza kuwa ni heshima kubwa kwa klabu.

“ Ni Heshima Kubwa kwa Klabu yetu kupokea mashindano ya PWC lakini ni heshima kutumia mashindano hayo kupima uwezo wa wachezaji waliochaguliwa timu ya taifa na mchujo wa wachezaji ili kupata idadi kamili ya wachezaji wanaotarajiwa kuwakilisha nchi.” Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja na wachezaji kutoka Klabu zote za golf nchini ambao mpaka sasa wamefikia zaidi ya 100 ambao wamethibitisha kushiriki na kuomba wadhamini zaidi kuendelea kujitokeza kusaidia mchezo wa golf kupitia Lugalo kwani Milango iko wazi.

Kwa Upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Japteni Masai alisema mashindano yanatarajiwa kuanza saa moja na nusu ambapo wachezaji wa Kulipwa,Wachezaji wa Timu ya Teule ya Taifa,Junior na wanawake wataanza.

Kapteni Masai aliongeza kuwa kundi la Pili la mashindano hayo yatakayoendeshwa kwa mtindo wa Mikwaju ya Jumla Stroke Play Net litaanza saa tatu asubuhi ambapo Wachezaji wa Ridhaa wote kwa makundi yote watacheza.

Kwa Upande wake Afisa Masoko wa PWC ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo Wilfred Nyaki alisema wanashukuru kupata fursa katika mashindano haya na wamechagua klabu ya lugalo kwa kuwa ni klabu bora nchini na wataendelea kufanya hivyo ikiwa sasa ni miaka mitatu nawanadhamini ili kutoa nafasi kukuza mchezo huo miongozi mwa jamii.

Nyaki aliongeza kuwa Maandalizi yote kwa Upande wa zawadi yamekamilika na kinachosubiriwa ni washindi kukabidhiwa na wanamatumaini makubwa na mafanikio ya siku hiyo ikiwemo Timu ya Taifa kupata wachezaji waliowakusudia.

Wachezaji wa Timu ya Taifa watakaothibitishwa baada ya mashindano ya PWC wanatarajiwa kuondoka nchini Jumanne Oktoba 25.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...