Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco,  Mtukufu Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa ziara ya kibinafsi.
Mfalme wa Morocco Mtukufu  Mohammed VI(kulia) akisalimiana na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga mara baada ya kuswalisha Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa ziara ya kibinafsi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi iliyotolewa na Mfalme wa Morocco  Mtukufu Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco Mtukufu  Mohammed VI, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka nje ya Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco Mtukufu a
Mohammed VI, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja. Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa ziara ya kibinafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...