Nteghenjwa Hosseah – Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepokea msaada wa bati 500 pamoja na mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati pamoja na shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Arusha.

Mara baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo, Gambo alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Dararro mifuko 100 ya saruji na mabati 100 kwa ajili ya ujenzi kituo cha afya kinachojengwa eneo la kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini Arusha.

Alisema msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao kwani kila wilaya za mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil – Jiangsu Joint Venture Ltd, inayojenga barabara ya Sakina – Tengeru Km 14.1 na barabara ya Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa msaada huo kama sehemu ya kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza mahusiano na kujali jamii na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi wa barabar hiyo itakayogharimu takribani Bil. 139.

“Naishukuru kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo na naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo na kila wilaya nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya kupunguza changamoto mbalimbali kwa jamii “.


Meneja Mradi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, Bw.Xie (kulia mbele) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mbele kushoto) mfuko wa saruji na bati kama sehemu ya msaada wa bati 500 na mifuko ya saruji 500 waliyoitoa kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za Maendeleo katika Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kushoto) akimshukuru Meneja wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, baada ya kuhakiki msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500. 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo (mbele) akishukuru Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd kwa kutoa msaada kwa wananchi wa Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo(mbele kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha mifuko ya saruji 100 na bati 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet. 

Mhandisi wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mkoa John Kalupale (kwanza kulia) akiwatambulisha wawakilishi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd walipokuja kukabidhi msaada wa mabati na Cement kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...