Serikali
imeyakabidhi makampuni ya mafuta ya OILCOM, GBP na MOIL hati za Ujenzi
wa Shule ya Sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la
ardhi mkoani Kagera lilitokea mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano wa hati hizo jijini Dar es Salaam leo Tarehe 23
Oktoba, 2016, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dkt.
Hamisi Mwinyimvua ameyashukuru makampuni hayo kwa ahadi ya kujenga shule
mbili zilizobomoka kutokana na tetemeko hilo.
“Shule
ya sekondari ya Ihungo na Shule ya Sekondari ya Nyakato zilibomoka
kutokana na tetemeko hilo, Kwa kuwa serikali imeanza kujenga shule ya
sekondari ya Ihungo ninawakabidhi nyaraka za ujenzi wa shule ya
sekondari ya Nyakato na ninaamini mtakamilisha ujenzi kwa wakati ili
wanafunzi waweze kurejea shuleni hapo”amesema Mwinyimvua
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor amesema makampuni yao
yataendelea kuziunga mkono juhudi za serikali za kukabili na kurejesha
hali pindi maafa yanapotokea nchini.
“Sisi
tunaamini nchi yetu ya Tanzania lazima ijengwe na watanzania wenyewe na
sisi hatunabudi kuwasaidia ndugu zetu wa Kagera kwa athari walizozipata
za tetemeko kwa kujenga shule hiyo kwa ramani ambayo mmetukabidhi” amesema Mansoor
Naye, Katibu
Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Bi. Maimuna Tarish
amesema kuwa jukumu la wizara hiyo ni kutoa elimu bora na ili elimu iwe
bora ni lazima iwepo miundo mbinu ya majengo ya shule ambayo ni bora
kama itakayojengwa na makampuni hayo ya mafuta.
“Tutawakabidhi
michoro ya shule hiyo ambayo ujenzi wake umezingatia ushauri wa
wataalamu wakiwemo wa Jiolojia, aidha katika ujenzi mtakao
kuwa mnaufanya Wakala wa majengo ya serikali (TBA), itasimsmia kazi ya
ujenzi ili kuhakikisha ubora unaotakuiwa unafikiwa” amesema Tarish
Itakumbukwa
kuwa nchi yetu ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika Kanda ya Ziwa na
Hasa Mkoa wa Kagera , Mwezi Septemba mwaka huu. Tetemeko hilo lilikuwa
na athari kubwa kwa miundombinu na majengo ya taasisi mbalimbali za
serikali na makazi ya wananchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, OKTOBA 23, 2016
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato, kutokana na hiyo na makumpuni ya mafuta mengine ya OILCOM na GBP waliahidi kuijenga shule hiyo iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardh mkoani Kagera, Septemba, 2016, makabidhiano hayo yamefanyika tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba , 2016, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu GBP Badal Sood, Mkurugenzi MOIL, Altaf Mansoor, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,Maimuna Tarish, tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...