Serikali imewataka watumishi wote nchini walioajiriwa na Serikali, yakiwemo mashirika ya Dini na Taasisi nyingine ambazo haziko kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya Serikali lakini zinapata ruzuku kutoka Serikalini; kuwa wamesajiliwa katika zoezi la Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma linaloendelea kote nchini, kufikia Oktoba 31, 2016.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, katika mkutano wa pamoja ulioitishwa kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Bi Kairuki amesisitiza; “waajiri na watumishi watakaoshindwa kutekeleza zoezi hili watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo”

Akifungua mkutano huo uliolenga kutoa tathmini ya mwenendo wa zoezi linaloendelea la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma lilioanza nchi nzima tangu Oktoba 03, 2016, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu L. Nchemba (Mb) amesema mpaka sasa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imefanikiwa kusajili zaidi ya asilimia 50% ya watumishi wote nchi nzima na baadhi ya mikoa kukamilisha usajili kwa zaidi ya asilimia 95%. Ameutaja mkoa wa Geita kuwa mkoa unaoongoza kwa kufanya vizuri katika zoezi hilo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba (Mb) akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari mkoani Dodoma kuhusu mwenendo wa zoezi linaloendelea la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) na Bi. Rose Mdami, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati, akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA 
Waziri akipokea maelezo ya namna shughuli za usajili zinavyo ratibiwa na ofisi ya usajili Wilaya ya Dodoma Mjini ; alipofanya ziara ya ukaguzi na kukutana na viongozi na watumishi wa Umma waliofika kupata huduma 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...