Na Mary Margwe, Simanjiro

Ili kuepusha kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi, halmashauri ya wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara imejipanga kikamilifu kuhakikisha inaondokana kabisa na migogoro hiyo, ambapo kesi zote za ardhi zitatatuliwa na mabaraza ya ardhi ya kijiji na kata bila kuingiliwa na watendaji ,wanasiasa, na wenyeviti ambao wameonekana kuingilia migogoro hiyo badala ya kuyaachia mabaraza husika kushughulikia utatuzi huo.

Ngazi ya chini kuna mabaraza ya ardhi ya kijiji na kata ambayo yapo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi,ambayo yamepewa dhamana ama jukumu la kukaa na kutatua migogoro hiyo bila kuingiliwa na watendaji, wanasiasa, wenyeviti , madiwani ili kuweza kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi zao,hali inayosababisha kuwepo na kuongezeka kwa migogoro mingi inayopelekea hata vifo kwa raia.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara Yefred Myenzi, alipokua akiongea kwenye baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, ambapo alisema tayari halmashauri yake imekwishatoa mafunzo maalum ya kila kiongozi kutambua majukumu na mipaka ya kazi anazotakiwa kufanya, hivyo ategemei kuona mwiingiliano wa majukumu hayo yakiendelea.
Myenzi alisema kamwe kukiwa na mwingiliano wa majukumu yoyoye yale, itakua ni vigumu kufikia muafaka wa jambo husika, kwani vipingamizi vitakua vingi vya kupinga jambo husika,hivyo ni vema kuepukana mapema na migongano ya majukumu na hata mwingiliano wa wajibu kati ya watendaji wa vijiji na kata, wenyeviti wa vijiji, wanasiasa ,watoa maamuzi ya haki, na madiwani kutojihusisha kabisa na utatuzi wa migogoro ya ardhi na badala yake wayaachie mabaraza ya ardhi ya kijiji na kata katika kukabiliana na changamoto hiyo na si vinginevyo.

"Waheshimiwa madiwani nyie kama wasimamizi wakuu wa shughuli za maendeleo katika kata zenu hivi mtajisikiaje pale mtakapoona viongozi wengine wanakuja kuingilia majukumu yenu, mtajisikiaje,hivyo Kila mmoja wetu ahakikishe anawajibika kikamilifu katika majukumu yake, bila kuingiliwa na mtu yaani kila mmoja atambue kipaka ya kazi zake,kwa kufanya hivyo tutakua tumeendana na taratibu,kanuni na sheria zetu ha nchi" alisema Myenzi.

Aidha alisema iwapo kuna mabaraza ya ardhi yasiyofanya kazi basi ni muda muafaka wa kuhakikisha yanaundwa upya ,yaliyokuwepo yaimarishwe ili yaweze kufanya kazi kikamilifu ndani ya mwezi oktoba,2016, kwa mujibu sheria.

"Naomba hili lifahamike waheshimiwa madiwani,usuluhishi wa migogoro ya ardhi kwa njia ya kimila naomba usiingiliane kabisa na taratibu za kisheria zilizowekwa kwa mujibu wa sheria za ardhi,kwani mabaraza ya ardhi yapo kwa ajili ya kutoa maamuzi ya haki kwa Kila mmoja,hivyo yasiingiliwe yameundwa kwa mujibu wa sheria tuyaachie tafanye kazi zao kwa uhuru" asisitiza Myenzi.

Aidha alimtaka kila kiongozi kwenye nafasi yake ahakikishe anafanya kazi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea suluhu ili zile zinazoweza kuishia ngazi ya kijiji, kata ziishie ngazi hizo, badala ya kila kero kupelekwa kwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi,jambo litakalowalazimu kurudi kwenye ngazi husika.

Migogoro mingi inaanziaga pale wageni ama raia wanapomilikishwa ardhi bila kufuata taratibu ,ambapo kwa mujibu wa sheria ni mkutano mkuu pekee ndio wenye mamlaka hayo, yaani ugawaji wa ardhi uzingatie taratibu za sheria na kuuridhiwa na mkutano mkuu wa kijiji na si vingine, ambapo mkurugenzi aliomba kupatiwa taarifa za wamiliki wa ardhi kwenye kijiji wenye mashamba makubwa zaidi ya ekari 50 awe hayo ofisini kwake.

"Serikali za vijiji haziruhusiwi kugawa au kumilikisha ardhi bila kuridhiwa namkutano mkuu wa kijiji, tena ni baada ya mjadala na kupitishwa kwa azimio la mkutano mkuubwa kijiji,ni marufuku kwa wenyeviti wa vitongoji kugawa ardhivwala wajumbe wa serikali ya kijiji bila maamuzi ya mkutano mkuu, ugawaji wa ardhi sharti ufanye na kamati ya huduma za jamii na shughuli za kujitegemea ambayo ni kamati ya kudumu ya serikali ya kijiji " alisema Myenzi.

Mbali na hayo aliwataka wenyeviti, watendaji kuhakikisha wanaitisha mikutano ya serikali ya kijiji Kila mwezi na mikutano mkuu ya kijiji Kila baada ya miezi mitatu, mikutano hiyo iandaliwe kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji mikutano yaani iwe na agenda zinazoeleweka kwa wananchi siku saba kabla ya mkutano zikiwa zimebandikwa mahala pa kazi ili kuwapa nafasi wananchi kujiandaa na mkutano,ambapo Kila kijiji kihakikishe kinakua na ratiba ya vikao na nakala yake itolewe kwa mkurugenzi mtendaji.

Hata hivyo mkurugenzi huyo a lot in a nafasi yake kupiga marufuku kwa wenyeviti wa vitongoji kumiliki mihuri na kunitumia kwa kuidhinisha mauzo ya ardhi wala shughuli nyingine ya serikali kwa kuwa wenye dhamana hiyo katika kijiji ni Afisa mtendaji wa kijiji na kata, na mwenyekiti wa kijiji, ambapo aliwapifa marufuku watu waliokua na dhamana ya uongozi wa kijiji hasa wenyeviti wa zamani kumiliki mihuri wala kunitumia kwa shughuli za serikali,itakapobainika hilo hatua kali dhidi yao itachukuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...