TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM

MAHAFALI YA KUMI YA TAASISI


Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) anawatangazia wahitimu na wadau wote wa DIT kuwa Mahafali ya Kumi ya Taasisi yamepangwa kufanyika Jumamosi tarehe 10/12/2016.

Mahafali haya yatatanguliwa na siku ya utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika mwaka wa masomo 2015/2016, sherehe ambazo zitafanyika Ijumaa tarehe 02/12/2016.

Taasisi inapenda kuwataarifu Wahitimu wote wa mwaka wa masomo 2015/2016 yaani wahitimu wa Shahada ya Uzamili (M.Eng), Shahada ya Kwanza ya Uhandisi (B.Eng.), na wahitimu wa Stashahada ya Uhandisi (OD) kusoma utaratibu wa kuthibitisha kushiriki Mahafali hayo katika tovuti ya Taasisi (www.dit.ac.tz)

“Rehersal” itafanyika Alhamisi tarehe 08/12/2016.

Wahitimu watakaoshiriki wanapaswa kulipia joho la Mahafali Tshs 50,000/= (kwa wahitimu wa  Shahada ya Uzamili – M.Eng) na Tshs 30,000/= (kwa wahitimu wa Shahada ya Kwanza (B.Eng) na Stashahada (OD) katika tawi lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145 na hatimaye kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi (www.dit.ac.tz).  Watakaoruhusiwa kushiriki Mahafali haya ni wale tu watakaokamilisha usajili wao.

ZINGATIA: Malipo yafanyike kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu wa mwaka 2015/16 iliyopo kwenye tovuti ya Taasisi, namba ya usajili na madhumuni ya malipo yaani Mahafali.

Mwisho wa kujisajili ni tarehe 15 Novemba, 2016.

Atakayeona tangazo hili anaombwa kumjulisha mwenzake.

Tangazo hili limetolewa na:

Ofisi ya Uhusiano,
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,
S.L.P 2958,

Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...