Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) kwa pamoja na Mhe. Florence Tinguely Mattli, Balozi wa Uswisi hapa nchini wakisaini Mkataba wa Makubaliano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uswisi kuhusu Ushirikiano wa Kisheria kwenye masuala ya Jinai. Mkataba huu utasaidia kuzijengea uwezo mamlaka zinazohusika na masuala ya Jinai na pia kubadilishana taarifa kuhusu masuala hayo. 
Mhe. Mahiga na Mhe. Mattli wakiendelea na zoezi la kusaini huku Maafisa kutoka Wizarani na Ubalozini wakishuhudia. Kulia aliyesimama ni Bw. John Pangipita, Afisa Mambo ya Nje na Bi. Sheila Ally.  
Dkt. Mahiga pamoja na Balozi Mattli wakibadilishana Mkataba mara baada ya kumaliza kuweka saini.
 
Tukio hilo pia lilishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka Luvanda (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Balozi Joseph Sokoine (wa pili kutoka kushoto), Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu na Bw. Pangipita (wa pili kutoka kulia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...