Benny Mwaipaja,WFM, Seoul, Korea 

WAFANYABIASHARA wakubwa kutoka KOREA ya Kusini, wamekaribishwa kuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda vitakavyoongeza thamani ya bidhaa za kilimo, mifugo, mazao ya bahari pamoja na kutumia malighafi zinazopatikana nchini ili kusisimua uchumi wa taifa na kukuza ajira. 
Wito huo umetolewa Jijini Seoul nchini Korea, na Mkurugenzi wa Uhamasishaji uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, JOHN MNALI, wakati akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika(KOAFEC). 
Mnali amesema kuwa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo kuondoa urasimu wa upatikanaji wa vibali vya kuwekeza na ardhi kwa ajili ya uwekezaji huo ili kuvutia mitaji na teknolojia kutoka nje ya mipaka yake. 
Amewashauri wawekezaji hao kufufua viwanda ambavyo havifanyi vizuri nchini, ili kuanza uzalishaji wa bidhaa zitakazotumia malighafi zinazopatikana nchini pamoja na kutumia soko kubwa lililopo katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na soko la AGOA la Marekani. 
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Sabra Issa Machano, amewahimiza wawekezaji wa Korea kwenda kuwekeza Visiwani humo na Tanzania kwa ujumla katika sekta za kilimo, viwanda na uvuvi wa samaki na mwani katika Bahari Kuu ili wakazi wa nchi hiyo na wawekezaji waweze kunufaika na rasilimali zilizoko visiwani humo. 
Amewahimiza wawekezaji hao kujenga hoteli za kisasa kwa ajili ya kuhudumia soko la utalii ambalo ni kubwa nchini humo, pamoja na kutumia mandhari ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao ni kivutio kikubwa cha watalii baada ya kutangangazwa na Shirika la Kimataifa linaloshughulika na masuala ya sayansi na utamaduni-UNESCO kuwa mji wa urithi wa Dunia. 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifuatilia kwa makini wakati Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania-TIC, John Mnali, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Seoul, Korea Kusini. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Utafutaji Rasilimali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar-Sabra Issa Machano.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, John Mnali, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.
Mkuu wa kitengo cha utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar, Sabra Issa Machano, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania Zanzibar, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akisalimiana na mwanafunzi wa Kitanzania anayesomea Chuo Kikuu kimoja nchini Korea Kusini kuhusu masuala ya biashara ya kimataifa na uchumi, Alice Mwamzanya, baada ya kushiriki mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul nchini Korea Kusini.(Picha na Benny Mwaipaja-Wizara ya Fedha na Mipango)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...